
THE LOVE HE NEVER PLANNED Mwandishi: Chieff Stories Mawasiliano: 0621045997 SEHEMU YA 14 Baada ya ile siku iliyojaa mabadiliko ya ghafla na mshangao mkubwa pale chuoni, moyo wa Leon ulikuwa umegawanyika mara mbili. Aliporejea nyumbani kwake, alisimama kwa muda mrefu mbele ya kioo kikubwa cha chumba chake cha kulala, akijitazama huku akijaribu kuondoa kwenye akili yake sura ya Nadia. Ili kuuvunja ule mtego wa kisaikolojia uliokuwa umeanza kumtawala, aliamua kubadilisha nguo haraka na kuchagua suti ya kisasa. Lengo lake lilikuwa moja tu: kwenda kusukuma mawazo hayo kupitia anasa za kupindukia kwenye klabu moja ya kifahari zaidi jijini. Alimpigia simu Jane
0 Comments