
Viana alikaa kwenye sofa na kuanza kusoma . Hiyo barua ilikuwa imeandikwa hivi. * JE UNA UHAKIKA NA UNAMUAMINI HUYO MWANAUME UNAEISHI NAE ? UNAAMINI NI KWELI ANA MAPENZI YA DHATI NA HATA KUUMIZA? UNATAKIWA KUWA MAKINI SANA KABLA HAUJAJUTIA. MASNA HUYO UNAEMUITA MFALME WA MOYO WAKO ALISHAMUACHA MALKIA WAKE WA ZAMANI KATIKATI YA GIZA NENE TENA BILA HURUMA YOYOTE. * CHUKUA TAHADHALI KABLA HAYAJAKUKUTA. Viana alimaliza kusoma na kujikuta anatetemeka. " Vipi baby nini kimeandika kwenye hiyo karatasi? " Kuna mtu ameandika vitu vya ajabu kuhusu wewe. Chriss alichukua ile barua na kuanza kuisoma. Alisoma huku akiwa amekunja uso
0 Comments