
BESTFRIEND MWANDISHI: Chieff Stories MAWASILIANO: 0621045997 SEHEMU YA 02 Maisha ya chuo yalikuwa tofauti kabisa na yale tuliyoyazoea tukiwa sekondari. Kila siku kulikuwa na watu wapya, mazingira mapya na majukumu mengi zaidi. Lakini kwangu mimi, kuna jambo moja lilikuwa bado lilelile. Kila nilipofika chuoni, nilijua siku yangu haikuwa imeanza vizuri mpaka nimemuona Reina. Siku hiyo nilifika chuoni mapema kidogo. Nilishuka kwenye gari langu na kuelekea kwenye jengo la lecture huku nikishika simu yangu. Nilikuwa bado naangalia baadhi ya meseji wakati nilisikia sauti nyuma yangu. “Allan!” Niligeuka na kumkuta Reina akija upande wangu akiwa na begi lake begani. “Umefika saa ngapi?”
0 Comments