BESTFRIEND 05

BESTFRIEND 05

BESTFRIEND MWANDISHI: Chieff Stories MAWASILIANO: 0621045997 SEHEMU YA 05 Siku chache baada ya Reina kuniambia kuhusu Ryan, hatimaye nilipata nafasi ya kumuona. Ilikuwa baada ya lecture. Mimi na Reina tulikuwa tumetoka darasani na tulikuwa tunaelekea cafeteria wakati Reina alisimama ghafla. “Allan, ngoja kidogo.” Nilisimama na kumtazama. “Nini?” Alitazama upande wa nyuma yangu kisha akatabasamu. “Yule pale.” Niligeuka. Kulikuwa na kijana mmoja amesimama karibu na jengo la lecture akiwa na wanafunzi wenzake. Alikuwa mrefu, amejipanga vizuri na alikuwa anaonekana mtulivu. Alipotuona, alitabasamu na kuanza kutuelekea. “Ryan?” nikamuuliza. Reina akatikisa kichwa. “Ndio.” Nilimtazama tena kwa sekunde chache. Kwa hiyo huyu ndiye Ryan.

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments