
BESTFRIEND MWANDISHI: Chieff Stories MAWASILIANO: 0621045997 SEHEMU YA 04 Baada ya Reina kuniambia kwamba alikuwa anataka kuanzisha mahusiano na kijana wa mwaka wa tatu, nilibaki na hamu ya kujua huyo kijana alikuwa nani hasa. Nilikuwa namjua Reina vizuri sana. Kwa hiyo nilijua lazima kulikuwa na kitu kilichomfanya amvutie kiasi cha kutaka kuingia kwenye mahusiano naye, hasa ukizingatia kwamba alikuwa hajawahi kudate kabla. Siku hiyo tulipokuwa tumekaa pamoja baada ya lecture, nilimwangalia na kusema, “Basi niambie huyo kijana anaitwa nani?” Reina alitabasamu. “Anaitwa Ryan.” “Ryan?” “Ndio.” “Yupo mwaka wa tatu?” “Ndio.” “Anasoma nini?” “Business Administration.” Nilitikisa kichwa huku nikijifanya kumchunguza kwa
0 Comments