
THE LOVE HE NEVER PLANNED Mwandishi: Chieff Stories Mawasiliano: 0621045997 SEHEMU YA 17 Baada ya siku kadhaa za kujitesa na kujaribu kupambana na hisia zilizokuwa zinamnyong'onyeza, Leon alishindwa kuimudu ile vita ya ndani na kujikuta akiangukia tena kwenye mfumo wa maisha yake ya zamani ya uhuni na starehe za kupindukia. Alianza kuonekana tena kwenye kumbi za kifahari akiwa na makundi yake ya kihuni, akitoka usiku wa manane na kubadilisha wanawake kama nguo ili tu kuzima lile wimbi la mawazo lililokuwa linamsakama. Hata hivyo, kipindi hiki alikuwa mwangalifu na mjanja zaidi; alihakikisha tabia zake chafu za usiku hazifiki hata kidogo kwenye
0 Comments