
THE LOVE HE NEVER PLANNED Mwandishi: Chieff Stories Mawasiliano: 0621045997 SEHEMU YA 23 Jemima, akiwa amesimama nje kwenye ukanda karibu na mlango wa darasa, aligeuka kwa haraka alipomwona Nadia akitoka. Macho yake yalikuwa yamejaa mshangao mwingi na maswali elfu moja yasiyo na majibu. Alimsubiri Nadia asogee karibu, kisha akamvuta pembeni kidogo kwa udadisi uliokuwa unamtesa. "Hivi alikuwa anakuambia nini huyo mwamba? Mbona wote mmebaki peke yenu ndani?" Jemima aliuliza kwa sauti ya chini huku akicheka kwa utani. Nadia alipiga chafya ndogo ya aibu, uso wake ukijaa joto ghafta huku akisema, "Acha utani wewe, alikuwa ananionyesha tu ile fomula ya pili
0 Comments