
THE LOVE HE NEVER PLANNED Mwandishi: Chieff Stories Mawasiliano: 0621045997 SEHEMU YA 22 Kipindi kile cha maswali na majibu kilisonga mbele kwa takriban saa nzima, huku kikiwa kimesheni uchangamfu mkubwa na uelewa mpana kwa wanafunzi waliokuwa wakihangaika na masomo yao. Leon alijitahidi kwa uwezo wake wote kufundisha kwa ufasaha, akihakikisha kila nukta inakaa sawa na kila kichwa kinapata kile kilichokosekana, ingawa ukweli ulikuwa wazi moyoni mwake kuwa lengo lake kuu halikuwa darasa zima, bali lilikuwa ni kumuona Nadia na kujua namna gani angeweza kumvuta karibu yake bila kuleta shaka. Hata hivyo, Nadia alikuwa kimya na mtulivu wa kipekee; aliandika kila
0 Comments