
05* MY HEART Nilifika ghetoni kwa Jabir, nilijizuia kuingia baada ya kukutana na bonge la Muziki, kama mnavyojua nyumba za Wanafunzi ni full vurugu tu. Inaonekana yeye na Washkaji zake walikuwa na party. Sikutaka kuwa kikwazo kwao, sauti za Wadada wakipiga kelele zilipenya masikioni mwangu na kwa namna fulani hivi nilijikuta ni kisikia wivu. Niliondoka kwa kutembea, sikutaka kusumbuana na dreva wa bajaji wala pikipiki. "Kwanini Jabir hajawahi kunitambulisha kwa rafiki yake hata Mmoja? kwanini asinialike kwenye party? kwanini hajawahi kuniuliza kuhusu changamoto nazokutana nazo kazini?" Nilijikuta nikijiuliza maswali mengi bila majibu "Kuanzia sasa na kuendelea sitamfuatilia Jabir, sitaenda kwake
0 Comments