
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋 Walipoondoka nilirudi ndani kwa huzuni. Nilimchukua Dalton na kwenda kulala nae chumba cha wageni sababu tusingeweza kulala kwenye chumba chake cha mwanzo maana kilikua kimefungwa camera. Tukiwa huko Dalton akawa huru na mimi na kurudi kwenye hali yake ya kawaida. Alinibembeleza na kunipa pole “Usiwaache wakuharibie mood mke wangu” alisema kwa sauti ya utani. Nikamtazama kwa macho ya huzuni “Lakini wameondoka kwa sababu yangu…” “No! Wameondoka kwa sababu ya mipango yao imefeli! Kwanza toka mwanzo hawakuwai kunipenda! Walinidharau sana na kunisema vibaya so mamaaa relax!” “Ok” Dalton alinionea huruma sana, taratibu akinipangusa machozi. “Usilie tena” Kisha akanilaza kifuani kwake
0 Comments