
ENDELEA..... Mama mdogo aliongea kama vile anamchamba. Mwanamiss alimtazama Samir Kwa kiulizo. "Ni kweli ni mke wangu. Sikutaka kukwambia Jana kwasababu ya hali Yako uliyokuja nayo". Samir aliongea hayo. Ukimya sekunde kadhaa ulipita. "Ninachowaomba tu muishi vizuri. Na hivi karibuni mmoja nitamtafutia nyumba nyengine". "Nadra haondoki humu ndani". Mama mdogo aliyasema hayo na kusababisha Mwanamiss amuangalia Kwa jicho Kali sana. "Hata mimi siondoke. Hapa ni kwangu. Nadra amenikuta, mie ndo mke mkubwa". "Tulishakusahau lakini, miaka karibia ishirini mchezo". Mama mdogo aliyasema hayo. "Haijalishi ila ndo nimeludi na mume wangu amenipokea pia, siwezi kuondoka humu ndani nikaishi nyumba nyengine". "Acheni mizozo".
0 Comments