
ENDELEA....... Baada ya kumaliza kuongea na mama kwenye simu nilianza kuutafuta usingizi. Majira ya asubuhi palikucha niliamka mapema na kwenda kusaidiana na dada wa kazi kupika. Kipindi icho nilikuwa nishaweza kupika japo sikuwa na jiamini kivile ila kwakuwa nilikuwa napenda kukaa jikoni kumtazama dada wa kazi qnavyopika basi ilikuwa rahisi na mimi kuweza kwa haraka. Tulikuwa tunapika huku tunapiga story mbili tatu. Tulikuwa tunezoeana na mdada wa kazi kama vile mtu na shoga Ake. Baada ya kumaliza kupika tuliandaa mezani. Nililudi chumbani kwangu. Muda mchache alikuja mume wangu alikuwa ashavaa nguo za kazini. Nilishangaa namna alivyovaa jamani. "Mbona umevaa hivi?".
0 Comments