
Niliongea na Eliza sana, yaani kidogo nilihisi moyo wangu sasa umepumua. Nilimuomba nilale akasema sawa kesho nijitahidi niwahi ili tuongee nikasema poa. Nilikata simu, kulikuwa na msg nyingi kweli za Karim, nikafuta bila hata kusoma mnafki tu huyu kaka. Nikaizima simu yenyewe nikajilalia zangu ila roho ilikuwa inanitukutia kweli, nakumbuka upendo ule wa agape alikuwa ananionesha jamani vile vicheko nilikuwa nae njoy sana kuwa nae, hata hivyo nilimpenda mnoo huyu kaka kabla hata sijajua kama atakuja kunifata. Sasa kwanini alinambia hana mahusiano na Edda? Niligundua hata mie nilijirahisi sana kwake, yaani huenda aliuona udhaifu wangu ndio mana alinipata kirahisi sanaaa,
0 Comments