
Kwa majina naitwa Bianca. Nimezaliwa Arusha huko ndani ndani. Simjui mama yangu wala baba; nimekuwa nikiishi na bibi yangu kwenye nyumba hata sijui ya nani. Bibi yangu ni mzee sana. Yaani tangu mdogo yeye alikuwa hivyo hivyo mzee. Maisha yetu yalikuwa magumu mno; magumu zaidi hata ya hayo magumu menyewe. Sikufanikiwa kwenda shule. Bibi yangu alikuwa akiishi kwa kuomba omba mitaani huku mimi akinibeba mgongoni na uzee wake. Tulizunguka mitaani na kwenye barabara kubwa. Nakumbuka siku moja, kipindi hicho tayari ninajielewa, nakumbuka nilikuwa kwenye miaka 6 hivi kwenda 7. Wakati huo nilikuwa nikimshika mkono bibi tunazunguka mabarabarani. Siku hiyo tukiwa
0 Comments