
Kweli Jack alikua kakumbatiwa lakini sio na Lucy. Baada ya Jack kumfuatilia Lucy kwa muda mrefu bila mafanikio akaamua amuache aendelee na maisha yake lakin alipata mchumba hapo hapo kwenye taasisi anayofanya kazi Lucy maana alikua akienda hapo Mara kwa mara..mwanadada huyo anaitwa Winny. Basi Jack aliamua kuanzisha mahusiano na Winny na akaachana kabisa na habari za Lucy na kuamua kufurahia mahusiano yake mapya ya yeye pamoja na winny. Wakati ambao Lucy alisema nitakupenda daima alikuwa ameshikilia picha ya mumewe Dickson na alikua karibu na alipo Jack na Winny maana walikuwa kwenye mgahawa uliokuwepo kazin hapo na hakuwa amekaa nao
0 Comments