
Ilipoishia eps 21 Tulikaa hapo Dubai kwa wiki nzima baada ya hapo tukarudi nyumban. Michael tulimkuta jaman tulipata Dada mstaarabu na kipindi chote tupo Dubai tulikua tukiwasiliana na Dada na Mara nyingi niliongea na Michael na alijua mimi ni mama yake kwa jinsi alivyokuwa ananipenda. Songa nayo.................. Dickson alitaman kunipa kila kitu alinifanya kuwa Kama malkia wa falme yake,alinidekeza sana. Ingawa alimkataa mtoto wa Joyce lakin alikua akimuhudumia maana kweli ilikua damu yake na mtoto alifanana nae sana sasa kumbe Joyce alijua Dickson hana mchumba na hana mpango wa kuwa na mwanamke. Baada ya Dickson kunipa cheo alikua ananipost sana
0 Comments