MOYO ULIOTUMIKA 02

MOYO ULIOTUMIKA 02

SEHEMU YA 02 Nilirudi nyumbani nikiwa mnyonge, moyo wangu ulilipuka baada ya kumuona Masele (Muuza duka) kaja kudai pesa yake. "Asubuhi namna hii unakuja kuchukua pesa.... Mimi siyo ATM ukichomeka kadi yako unaondoka na pesa, kaendelee na shughuli zako nitakuletea muda niliochukua mafuta" Niliongea "Mtaa mzima umeujaza madeni laiti ningejua wala nisingepokea chupa yako kuweka mafuta" Masela aliongea kisha akaondoka Maneno yake hayakunishtua, kila nikilikumbuka busu la Jabir nilihisi ganzi mwili mzima. Nilihitaji kutafuta kazi ili niweze kumsupport Jabir wangu kwa namna moja au nyingine.....nilitamani kwenda nje kabisa ya Jiji la Mini kusaka pesa, changamoto iliyo nikabili ilikuwa ni nauli.

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments