
Nilisikia sauti ya mama akimwambia Manka tena kwa ukali, nikasema safiii bora kamsikia anipishe. Mimi vile nina hasira zangu basi tu .. Niliinuka nikaingia chumbani kwangu nikawa nimechukua kitabu changu nasoma taratibu. Mlango ulifunguliwa, nilipo inua uso nilisikia sauti ya mama akanambia ni mimi hapa Bianca. Alikuja mpaka nilipokaa akanikumbatia. "Mvumilie kidogo Sadru, huwa anaukorofi huyu mtoto lakini sintaruhusu akunyime raha sawa." "Hamna mama, mbona mimi nipo sawa. Hata kaka Sadru naamini atakuwa tu sawa na mimi na tutaishi vizuri, usiwe na wasiwasi mama," nilimjibu huku natabasam akanambia njoo tupate chakula cha familia, aliniinua akawa amenishika mkono tukashuka chini wote.
0 Comments