
Asubuhi nilikuwa nikifua, nafua na nguo za Sadru pamoja na zangu, nanyoosha vizuri ndio naondoka shule. Hayo maisha nilikuwa nimeshayazoea tayari na wakati huo kama Sadru alianza kunielewa maana alikuwa ananiongelesha vizuri hata kucheka anacheka na mimi. Sijui kwanini Manka alikuwa hanielewi kabisa, yaani kitendo cha kaka Sadru kuongea na mimi vizuri kwake ilikuwa kero sana. Alikuwa haishi kunisema sema yaani vimaneno maneno, mimi nikawa nakausha tu. Wikendi tulikuwa tunatoka wote na mama pamoja na Sadru maana mwanzo alikuwa hataki kabisa hata kuwa karibu na mimi. Maisha ya pale tena nikaanza kuyafurahia angalau nilikuwa natabasamu hata mbele ya kaka. Nakumbuka
0 Comments