MREMBO KIPOFU 09

MREMBO KIPOFU 09

Mapenzi yale ya mama ya mwanzo yaliisha kabisa, yaani yaliisha. Baba ndo usiseme maana alikuwa kila akija kutoka kazini lazima aongee na mimi, kama kuna kitu nahitaji au maendeleo yangu shuleni. Lakini hivyo vyote sikuviona kabisa, hakuwa ananiita hata nimsalimie maana baba alikuwa akichelewa sana yeye kutoka kazini kuliko wote, na kipindi hichi alikuwa amesafiri safari ya gafla sana. Nimekuja kujua kama baba amesafiri siku ya nne, hapo ndo nilijua mimi tena sina umuhimu kwa baba, kila alipopata safari alikuwa ananichukulia kama binti yake kweli, lazima aniage na kuniuliza nikuletee zawadi gani?? Sadru alisema mara kadhaa yeye atahama nyumbani pale.

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments