
Wakati huo wote tunaongea kaka alikuwa amenikumbatia tena vizuri kabisa wala sio kinafiki. Nikamwambia: "Mimi nilienda jikoni kumuu...." "Nyie kuna nini huku???" Sauti ya mama ndio ilinikatisha kuongea, nilijitoa haraka karibu na kaka nikasogea pembeni. "Hapana tunaongea tu, mmepata huduma ??" kaka aliongea huku anasogea alipo mama. Mimi niliona aibu kutokana na pozi tulilokuwa, japo kuwa ni kaka yangu lakini mwili wangu ulikuwa unahisi kabisa kuwa yule ni kaka maana hata mama alivyotukuta nilikuwa naona aibu. Mama alimwambia Sadru aende kukaa na Manka, akanivuta mimi pembeni. "Kuna nini kinaendelea wewe na Sadru??" Mama aliniuliza huku amekaza sauti. "Hamna kitu." "Mlikuwa
0 Comments