
Yaani hata sijui mkewe ilikuwaje akaja mule, mi nilikuwa kushtuka navutwa nikaanguka chini kama mzigo. Wakati najiuliza nini hiki mana ilikuwa gafla sana, nikasikia mumewe anasema, "We mama pili huoni utamuumiza mwenzio," aliongea sauti ya kufoka kwelii. "Maraya wewe, nilijua tu unatembea na mume wangu, niacheee nimesema niachee aumie tu mpuuzi huyu." Yule dada alikuwa akinipiga magumi pale pale chini, mumewe nae alikuwa anamvuta. Alipo fanikiwa tu kumtoa niliwahi nguo haraka nikajifunga, hapo majirani walishasogea. Alikuwa anachamba kweli, anasema anajuaga muda mrefu kuwa natembea na mume wake leo amenifumania tena chooni. Mumewe akamvuta wakapelekana ndani. Niliingia chumbani huku naona aibu,
0 Comments