
Sadru alinielezea jinsi walivyokuwa wananitafuta mimi wasiwasi waliokuwa nao juu yangu. Wakati huo tulikuwa njiani ananipeleka nyumbani, nilimuelekeza mpaka tukafika. Akaniambia umekuja kujichimbia mbali sana daah, kumbe Dar kubwa hivi, mi nilikuwa nacheka zangu tu. Wakati huu ilikuwa mida ya jioni jioni hivi, kati ya watu tulio wakuta pale alikuwepo mama mwenye nyumba pia na yule dada na mumewe na mwenyekiti. Yaani nafika tu ananiambia tumekusubiri sana Bianca, tulikuwa tunakaribia kugairi kikao. Aah, ndo nikakumbuka asubuhi niliacha uporo, sikuwa hata na shida na kikao chao, kwanza nimempata Sadru akuu. Niliwaambia nakuja ngoja nimfikishe mgeni wangu ndani. Sadru alikuwa anashangaa mazingira
0 Comments