
Nilishindwa kunyamaza, yaani leo ndo mara ya mwisho kuona ulimwengu wenye giza, kesho naona tena dunia, naiona tena dunia mimi?? Eeh Mungu wee jamani, Mungu wanguu Sadru nikupe nini mimi ujue nina furaha kiasi gani! Mungu akulinde Sadru, akupiganie sana Sadru, sala zangu zitakuwa nawe mpaka pumzi yangu ya mwisho. Nilikuwa nawachukia mno wanaume lakini Sadru nilitamani awe hapa, yaani karibu yangu kabisa. Tulishinda na Sadru siku nzima, alikuwa ameshika mkono wangu ameketi pembeni ya kitanda changu. Alinipigisha story nyingi sana, tulikuwa tunacheka, ilikuwa siku nzuri mno. Usiku Sadru hakutoka, alilala pale pale. Nakumbuka nilikuja kuchukuliwa asubuhi na kupelekwa moja
0 Comments