
Yaani hapo sielewi gari zote naziona nzuri nichague ipi mie tena sielewi nikamwambia mi hata kuendesha gari jamani sijui akanambia utajua tu we angalia hapa unayoona nzuri kama huoni twende sehemu nyingine jamani. Kuna yule dada alikuwa anatutembeza kuangalia magari ndio akaanza kunidadavulia kila aina ya gari iliyopo pale huku akinishauri ipi nzuri zaidi ipi kwa mwanamke inapendeza basi mwisho nilichagua kigari matatizo kikali hicho hatari, akalipia akaomba itufate nyumbani jamani. Tukaenda kwenye duka kubwa la nguo akanichukulia nguo na viatu kiwigi make up, tukaenda home nikaikuta gari tayari ipo ndani nilitamani kuishika shika lakini nikavunga mwenyewe mana kuna mlinzi
0 Comments