
Ukali uliokuwa unatawala kwenye chumba kile cha chakula ulikuwa mzito kiasi kwamba hata hewa ilionekana kusimama kwa sekunde kadhaa. Mikono yao ilipokutana, mkono wa Tariq ukiwa umeshika kiganja cha Tahiya ili kuzuia asitupe kile kikombe cha chai, umbali uliokuwepo kati yao ulikuwa mdogo sana kiasi kwamba Tahiya alianza kusikia harufu nzuri ya marashi ya kiume yaliyochanganyika na harufu ya asubuhi ya mlinzi huyo. Tahiya alijitahidi kuweka ugumu, akakunja uso wake kwa hasira iliyoigizwa huku macho yake makali yakijaribu kutishia, lakini moyo wake ulikuwa ukidunda kwa kasi isiyo ya kawaida. Alikuwa amezowea wanaume waliomnyenyekea, waliokuwa tayari kulamba vumbi miguuni pake pindi
0 Comments