
Mvua kubwa ilikuwa ikipiga kwa fujo kwenye madirisha ya jumba hilo la kifahari, huku upepo mkali ukitikisa miti iliyokuwa nje ya bustani ya Oysterbay. Ndani ya chumba cha Tahiya, giza lililotokana na kukatika kwa umeme liliongeza hofu kubwa moyoni mwake. Kila mara radi ilipopiga na kuwaka kwa mwanga mkali wa bluu, Tahiya alikuwa akijikunyata zaidi kwenye kona ya kitanda chake, mikono yake ikiwa imezuia masikio yake huku akitokwa na machozi ya hofu. Tangu utotoni, alikuwa na phobia kubwa sana na miangaza ya radi na sauti zake za kishindo, na mara zote alipokuwa akisikia mvua ya namna hiyo, mama yake au
0 Comments