
Mvua ilikuwa imekata kabisa nje, ikiacha baridi hafifu la usiku wa manane ambalo lilibembeleza mtaa mtulivu wa Oysterbay. Ndani ya chumba kile cha kifahari, hewa ilikuwa bado imetawaliwa na joto la mwili wao na harufu nzuri ya marashi yaliyochanganyika na jasho jepesi la mahaba mazito waliyotoka kuyashiriki. Tahiya alikuwa amelala kifua kipana cha Tariq, kichwa chake kikiwa kimetulia vizuri kwenye bega lake huku vidole vyake vya mkono wa kulia vikichezea nywele fupi za kifua cha mwanaume huyo kwa mtindo wa mahaba. Mapigo ya moyo ya Tahiya yalikuwa yatulivu lakini yaliyojaa mshangao mkubwa juu ya kile kilichotokea usiku ule. Mwanamke ambaye
0 Comments