
Asubuhi ya siku iliyofuata ilifika kukiwa na hali ya hewa ya baridi kidogo iliyoacha alama za mvua ya usiku uliopita mitaani mwa Oysterbay. Jua lilichomoza taratibu likitoa miale ya dhahabu iliyopenya kupitia madirisha makubwa ya kioo ya jumba la marehemu Mzee Bwire. Tahiya aliamka akiwa amejipumzisha kwenye vifua vya Tariq, mikono yao ikiwa bado imefungana kwa mahaba mazito ya usiku uliopita. Lakini amani hiyo ya asubuhi haikudumu sana. Mlango Mkuu wa jumba hilo ulisikika ukibishwa kwa nguvu na kwa fujo, ikifuatiwa na sauti nzito za watu waliokuwa wakisema kwa mamlaka sebuleni. Macho ya Tahiya yalifunguka kwa kasi kubwa, hofu ikimvaa
0 Comments