
Siku nzima shuleni Naila alikuwa akinisusia. Nilikuwa na hasira dhidi ya alichokifanya Rex kwa rafiki yangu na kwa Mansour. Nilipotoka shule, Bahati nzuri mama akaaga anaenda kwa shoga yake mama Rashidi, nami bila kupoteza muda nikatoka nduki kuelekea kwa Rex! Niligonga mlango kwa nguvu jamaa akafungua nusu, akanitazama kama hanijui vile. "Unataka nini Raya?" "Naomba tuongee” nilimwambia kwa msisitizo. Ndipo Akafungua mlango wote, akaniruhusu niingie ndani. Tulipofika sebulei sikujivunga nilimjia juu sikutaka mchezo kabisa "Kwanini umefanya vile Rex?! Kwanini?" "Nimefanya nini?" aliniuliza kama hajui "Kumpiga Mansour?! Bora hata ungempiga huyo Mansour maana hana faida yoyote kwangu, lakini kwanini umempiga Naila?!"
0 Comments