
Sikusubiri hata Mansour aongeze neno lingine, nikaikata chap kabla hajaniharibia zaidi! Mama alinikodolea macho "Kwanini umekata simu Raya?!"😳 "A-atakuwa kakosea namba huyu bwana!" "Si umesema hapa anayepiga ni rafiki yako?" mama alizidi kubana. "Ndio mama... Nilidhani ni Naila!" nilijitetea "Usinifanye mimi mtoto mdogo Raya! Nimeona kabisa ume-save Mansour!……Umeanza mambo ya wanaume eh?!" "Hapana mama, sio hivyo..." Mama hakutaka maneno mengi, alivuta ndala akanizaba tatu za chap chap za mgongoni! Weeeh maumivu yalikua balaa, kabla sijakaa sawa akanipiga za mkononi kama hana akili nzuri. Nikawa nalia naomba msamaha nikasema hapa nikikaa vibaya nitapigwa mpaka nijinyee! Niliamka speed speed nikakimbilia ndani kujifungia.
0 Comments