
_______________ SEHEMU YA SITA Chriss alikaa kwenye sofa la mbele akiwa bado anamkodolea macho Jenipha kwa tabasamu la kuvutia, wakati huo Jenipha alikuwa akimuangalia kama vile anaona aibu flani , hiyo hali ilizidi kumvutia sana Chriss na kufanya kuhoji maswali ili kujenga ukaribu nae. "Umekuwa rafiki wa Viana kwa muda gani?" aliuliza huku akijaribu kuanzisha mazungumzo. "Ni muda sasa, tumesoma pamoja... tumepitia mengi pamoja," alijibu Jenipha kwa sauti ya taratibu, yenye mvuto. "That's nice. Karibu sana hapa, jisikie kama upo nyumbani." Jenipha alicheka kidogo kisha akasema, "Asante Chriss, naona tayari kama niko nyumbani... kwa mtu kama wewe, siwezi kujisikia vibaya."
0 Comments