VIANNA 🥰🥰💃 ( Binti aliyebadilisha maisha ya playboy wa kizungu ) 11

VIANNA 🥰🥰💃 ( Binti aliyebadilisha maisha ya playboy wa kizungu ) 11

_______________ SEHEMU YA KUMI NA MOJA Kuna hisia ambazo hakuwahi kuzipata hapo nyuma zilimfanya Viana atulie na kujiona mwili wake ukisikia, Baada ya muda ni kama fahamu zilimrudia Viana alishituka na kujitoa kwa nguvu kwenye mikono ya Chriss kisha akamuangalia usoni. " Samahani, sikudhamiria kufanya hivyo. Viana hakujibu kitu alienda kuchukua kisu anamkabidhi, Chriss alienda chumbani na Viana akaendelea kufanya kazi zake lakini lile tukio lilikuwa likijirudia kichwani kwake. " Mmmmh sijui aliwaza nini mpaka akamkumbatia vile, mmmh naijuia hiyo na mimi nipo ngangari sitegeji ng'o naona sasa anataka kuhamia kwangu mimi sio wa hivyo. Viana hakuwa na imani kabisa

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments