
SEHEMU YA 7 "Tumekuona umeongozana na dada mmoja ni mfanyausafi mpya?" Hellen alimuuliza Bella, frida nae alisogea kusikiliza jibu la Bella "Mmmh nikiwaambia cheo chake wote mtabaki mdomo wazi" Bella alivuta kiti akakaa "Tuambie basi" alisema Frida "Yule ni secretary mpya ..Yani tutakuwa tunasaidiana kazi" Bella aliweka kituo "Eti nini ? Kweli Mr Merrick ameanza kuwa na makengeza Sasa yule mwanamke mbona haendani kabisa na hiyo kazi kwanzia kuvaa na kila kitu" hellen aliongea kwa mshangao "Achaaa shoga angu amekaa mswahili Swahili tu na nilivyosipendi mtu anaeongea sana" Bella aliongea kwa kulalamika "Sasa utafanya nini shoga angu?" Frida alimuuliza Bella
0 Comments