
THE LOVE HE NEVER PLANNED Mwandishi: Chieff Stories Mawasiliano: 0621045997 SEHEMU YA 21 Siku ya kikao cha marudio ya maswali ilipowadia, hali ya hewa ndani ya lile darasa dogo ilikuwa ya uchangamfu. Wanafunzi wa mwaka wa kwanza walijitokeza kwa wingi wakiongozwa na yule Class Representative (CR), ambaye alikuwa amejipanga na daftari lake lenye maswali mengi magumu yaliyohitaji ufafanuzi. Wakati wanafunzi wakiendelea kutulia na kukaa kwenye viti vyao huku wakisubiri, mlango ulisukumwa taratibu na Leon akaingia akiwa amevaa mwonekano wa kuvutia lakini wa kistaarabu zaidi tofauti na siku zilizopita. Macho ya wanafunzi wote yalitua kwake, na minong'ono ya siri ikaanza kusikika
0 Comments