
Msanii Mkongwe wa bongo fleva Dudu Baya amesema kuwa kutokana na ushauri aliopewa na Mambaz Genz ameamua kutengua kauli yake aliyosema kuwa hatoshiriki show za miaka 30 ya bongo fleva Mikoani. Dudu Baya amedai kuwa Mambaz 24 inamashabiki wengi duniani hivyo wangependa kumuona kwenye show za mikoani hivyo akaamua kukubaliana nao. ''Baada ya tamasha la tarehe 10 mlimani city nilitoa uamuzi mkali sana yakwamba show zinazofuata mikoani sitashiriki nilivyotoa tamko mambaz 24 wa mikoani hawakufurahishwa na hivyo kwa demand ya mambaz wote duniani walisema tunataka tukuone nakubaliana na nyinyi mambaz 24 nitashiriki miaka 30 ya bongo fleva mikoani''Amesema-Dudu Baya Mwana
0 Comments