
FALLING FOR MAID SEHEMU YA 0 7 Nilishtuka sana, nikauliza kuwa amepata ajali ya nini, akaniambia kuwa alipotoka pale nyumbani alienda kuvaa mti, so ndiyo kakimbizwa hospitali. Nilitamani nipae niende huko hospitali nikamuangalie anaendelea aje, ila nikasema nitulie, maana mimi ni mfanyakazi, tena mfanyakazi ambaye silipwi bali napewa chakula na malazi bure, huo ndiyo mshahara wangu, alafu nianze kuleta kiherehere, nikaona bora nitulie tu. Nikiwa nimekaa zangu sina hili wala lile, mara nashangaa Vannessa huyo anakuja, alipofika akaanza kuniangalia kwa dharau kisha akasema, “Hivi unajua wewe huna maajabu kabisa.” Nikashangaa kwanini ananiambia vile na wakati hata hatujawahi kugombana hata kwa
0 Comments