
ENDELEA....... Samir alianza kupiga hatua kuelekea upande wangu ila gafla aligeuka na kumludia mwanae. Alimfuata mwanae pale chini na kumbeba haraka Kwa mikono miwili. Najma na dada wa kazi waliambiwa wasaidiane kunibeba Mimi. Samir alitoka nje akiwa amebeba mwanae. Walifika paki ya magari alimpandisha mwanae mlango wa nyuma na yeye kupande mbele. Kabda hajaliondoa gari alisikia sauti ya mwanae ikimuita. "Baba!". Aligeuka nyuma haraka kumsikiliza ila ashangaa baada ya kumuona Samir amekaa akiwa mkavu haswaaa. Sio yule aliyekuwa analia Kwa maumivu Makali. "Samira!". Samir alimuita mwanae Kwa mshangao. Samira hakumjibu baba yake zaidi ya kushuka kwenye gari na kuelekea ndani.
0 Comments