
ENDELEA...... Jafari alikuwa ananiangalia kwa kutabasamu. Mume wangu na mama mkwe wangu walioniona nilivyomwaga Ile Juice walisogea eneo la tukio. Mama mkwe alimuita dada wa kazi na kumwambia aje na Tambara. "Upo sawa mama Samira?". Mama mkwe aliniuliza. "Ndiyo?". Niliitikia ila ukweli akili ilikuwa ushavulugika kabisa. Macho yangu Bado yalimtazama Jafari na nilikuwa najiuliza inamaana Jafari ndo mchumba wa Samira au amekuja hapa kama mgeni, inawezekana kaja kwaajili yangu maana mala ya mwisho nilifungia namba yake na Wala hakunitafuta Tena. Nilishtuliwa na dada wa kazi aliniambia nisogee afute pale nilipodondosha Juice. Nilipiga hatua ila bahati haikuwa yangu. Nilikanyaga kichupa mguuni.
0 Comments