
ENDELEA.... Samira alisikia vizuri maneno yangu. Alifungua mlango nilishtuka na kutaka kuondoka. "Umesikia alichosema huyu mama Yako wa kambo?, kwanza anapata wapi nguvu ya kumpiga mkwe wake pasipo kumkosea Kwa chochote?". Jafari aliongea hayo. Wallah nilijisikia vibaya nilijikuta machozi yananitililika mashavuni. "Samira aliniangalia jicho la chuki, nilipotaka kumshika mkono alinisukuma kidogo nianguke. Samira alimfuata Jafari Alimkumbatia na kusema maneno haya. "Tafadhali usije ukaniacha Hassan wangu. Nakupenda sana". Masikini Samira alikuwa amezama mazima kabisa. Jafari alinitazama na kunikonyeza ishara hata nifanyaje siwezi kumzidi Kwa ujanja. "Nakupenda Samira wangu. Siwezi kukuacha mama. Piga uwa garagaza sikuachi ng'ooo!. Waliachiana kwenye kumbato. Jafari alimwambia
0 Comments