
Mtunzi....................Zooper ILIPOISHIA......... Mama Lulu alishituka baada ya kuona sura ya mtu aliyeoneshwa na mwanae na alijikuta mkono wake ukishika kifua chake kwa kupima mapigo ya moyo wake jinsi yalivyokuwa yakidunda.......... ENDELEA...... Mama Lulu alishangaa kuona picha ya mwanaume aliyepotezana nae miaka mingi iliyoweza kupita enzi za ujana wake na aliichukua simu ya mwanae ili apate kuhakikisha zaidi. "Mama mbona umeshangaa hivyo au unamfahamu huyo mtu!?" "Ha...pa..na simfahamu" Mama Lulu aliongea kwa shida huku ndani ya moyo wake akiwa na siri ambayo hakutaka kuongea mbele ya binti yake kwa wakati huo. Mwisho aliamua kunyenyuka nakuondoka huku Lulu akishangaa kwa mabadiliko aliyokuwa
0 Comments