
Rex hakufanya kitu kama nilivyo dhani, zaidi aliniuliza "Una hakika Raya?" "N-ndio... nina uhakika” nilijibu kwa kutetemeka vibaya mno. "Poa” Alifungua mlango taratibu akaondoka kimya kimya bila kuleta vurugu wala kusema neno jingine lolote. Mnajua sikuamini?? Maana nilidhani jamaa angekataa au angeleta vurugu pale ila haikua ivo. Nilishukuru Mungu na mimi nikafungua mlango nikatoka chumbani ili kuhakikisha kama kweli ameondoka. Nikagundua kweli aliondoka tena alipitia mlango wa sebuleni ambao ndo aliutumia kuingia ndani. Ukiniambia aliwezaje kuufungua mpaka leo sijajua bado😩. Niliufunga ule mlango chap kwa ufunguo, Ile nageuka tu nyuma Nakutana uso kwa uso na mama amesimama ananiangalia "We Raya!
0 Comments